HIVI NDIVYO VIWANGO VIPYA VYA NAULI BONGO



Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini (SUMATRA) imetangaza viwango vipya vya nauli kwa mabasi yanayokwenda mikoani, daladala na usafiri wa reli ya kati ambavyo vitaanza kutumika kuanzia April 12 2013 kutokana na gharama za uendeshaji kuongezeka.

Hivi viwango vipya vya daladala vimeongezeka kwa asilimia 24.46 huku vya mabasi ya masafa marefu vikiongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, asilimia 16.9 kwa mabasi ya daraja la kati na asilimia 13.2 kwa mabasi ya daraja la juu.

Kiwango cha chini cha nauli ya daladala kitakua ni shilingi 400 kwa abiria ikiwa ni umbali wa kilomita 10 na cha juu ni shilingi 750 kwa kilomita 26 hadi 30 huku mwanafunzi kwenye viwango hivi vipya akitakiwa kulipa shilingi 200.

Kwenye upande wa usafirishaji wa Abiria kwenye reli ya kati, nauli imepanda kwa asilimia 25 kwa daraja la kwanza na la pili huku daraja la tatu ni asilimia 44.
Previous Post Next Post