DON JAZZ JIBU ALILOJIBU ALIPOULIZWA KAMA KAMMIS D’BANJ


.

Zimebaki wiki kadhaa kabla ya mwaka mmoja kutimia toka ilipotangazwa kutengana kikazi kwa mastaa wa Nigeria D’Banj na aliekua producer wake Don Jazzy wa Mo Hits Records Nigeria lakini bado stori za kuachana kwao kila wakati zinaandikwa na Wanigeria lakini kwa engo tofauti.

Pamoja na hilo kwenye show ya Mchekeshaji AY wa Nigeria iliyofanyika juzi, Don Jazzy aliulizwa swali la kumchokonoa kuhusu kummis D’Banj kwa kipindi chote toka kila mmoja afate njia yake ambapo alimjibu mtangazaji aliemuuliza kwa kusema… “D’Banj anafanya vizuri popote alipo, unaniwekea maneno mdomoni mwangu lakini ni sawa, ndio… nimemiss D’Banj”

.
Previous Post Next Post