EXCLUSIVE: PASTOR MYAMBA AKIZUNGUMZIA JUU UCHAWI ULIOTUMIKA KWENYE MOVIE YAKE YA GOD'S KINGDOM



Mwigizaji mkongwe na anayefanya vizuri sana kwenye tasnia ya filamu Tanzania Emmanuel Myamba maarufu kama Pastor Myamba, alifanya mahojiano na Bongo61 Team juu ya filamu yake mpya ya God’s kingdom atakayoizindua rasmi taerehe za mwanzoni mwa mwezi wa Mei. Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayoa yaliyofanyika ndani ya ofisi ya Chuo chake cha maigizo na filamu cha T.F.T.C Kilichopo ubungo Dar es Salaam.

Bongo61 Team: Tungependa kujua ni nini hasa kipo ndani ya filamu hii yako mpya ya God’s Kingdom.

Pastor Myamba: Aaah, kwa kifupi, God’s kingdom ni filamu inayoonesha uweza wa Mungu ndani ya maisha ya mwanadamu. Ni filamu inayyonesha ni jinsi gani Mungu ni mkuu na muweza wa yote tofauti na watu wengi wanayodhani kuwa mtu au kuna kitu kinaweza kumshinda Mungu.

Bongo61 Team: Kwanini umeamua kutengeneza filamu hii?

Pastor Myamba: Filamu hii ni mahususi kwa watu wanaoamini kuwa unaweza kumshinda Mungu kwa kutumia uchawi. Nataka watu waelewe kuwa Mungu ni zaidi ya kila kitu. Na nguvu za Mungu ni kubwa na ndio zenye mamlaka zaidi.

Bongo61 Team: Umeshirikiana na nani katika filamu hii?

Pastor Myamba: God’s kingdom imefanya kwa ushirikano na Patcho Mwamba na Jengua pamoja na baadhi ya wanafaunzi wa T.F.T.C.

Bongo61 Team: Huoni kuwa filamu hii inaweza kuleta mtafaurku kwa watu wanoamini mambo ya kishirikiana?

Pastor Myamba: Mmmh, unajua mimi kama msanii nina haki ya kuigiza kile nachoomini ni sahihi kwangu, filamu hii haijamlenga mtu yoyote, mimi kama kioo cha jamii natakiwa kuonesha kile ambacho naamini ni sahihi kwa jamii kukifuata.

Bongo61 Team: Kitu gani kingine ungependa kuwaambia mashabiki wako?

Pastor Myamba: Wakae tayari kushudia vipaji vipya toka katika chuo change cha sanaa na pia kwa wale wanaotaka kujifunza zaidi kuhusu sanaa na maigizo nasi wanakaribishwa sana kujiunga nasi ili wapate mafunzo bora ya kuwa waigizaji wazuri hapo baadae.

Bongo61 Team: Tunashukuru sana, na kila la kheri

Pastor Myamba: Asanteni sana.
Previous Post Next Post