Chegge, Naumia kichwa


Msanii toka kundi la TMK Wanaume Family Chegge Chigunda amesema kwa hivi sasa hataki kufanya biashara yoyote baada ya kugundua zinampasua kichwa.

Katika siku za nyuma Chegge aliwahi kufungua duka la nguo ambalo lilikuwa likiuza nguo za wanaume na wasichana maeneo ya Kinondoni, baadae msanii huyo pia alikuja kufungua saloon ya kiume lakini nayo haikukaa kwa muda mrefu ikafungwa.

Chegge alisema kuwa sababu za kuamua kutokufanya biashara tena nikutokana na ugumu aliopata kusimamia biashara hizo hivyo kumpa hasara,

"Biashara inaumiza kichwa sana, mtu unawezeka pesa yako lakini ukija kupiga mahesabu unakuta ni hasara tu ndo maana nimeamua hivi sasa niachane nazo."
Previous Post Next Post

Popular Items