Mercy aanza mazoezi


Muigizaji nyota wa Nollywood Nchini Nigeria Mercy Johnson au Mrs. Okojie ameanza kufanya mazoezi ya kupunguza unene baada ya hofu kumuingia nyota huyo kuwa anaweza akampoteza mume wake kutokana na umbile lake hilo.

Mercy ameonekana kuanza mazoezi hayo ya kupunguza unene baada ya mumewe kuanza kumwita mwanamama huyo jina la 'Orobo' yaani bonge, na neno hilo limeanza kumkera Mercy ndipo ameamua kuingia gym ili kupunguza unene.

Ni majuzi tu Mercy na mumewe wamerudi nchini Nigeria baada ya kukaa kwa muda wa miezi sita wakitokea nchini Marekani ambapo alienda kujifungua mtoto wa kike anayefikia miezi sita sasa aliyepatiwa jina la Purity Okojie.

Mercy ameweka wazi kuwa anajiweka fit pia kwa jili ya kuanza rasmi kuingia katika uigizaji mwezi ujao
Previous Post Next Post