117 USD MILIONI ZATENGWA KWA AJILI YA BAJETI YA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI


Mahmoud Ahmad, Arusha
Jumla ya  dola za Kimarekani million 177,238,966 zimetengwa kwenye bajeti ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa mwaka wa fedha 2013-14 na kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo kwenye kikao chao cha 26 dharura kilichoisha leo  jijini hapa.
Mbali ya bajeti hiyo mkutano huo ulioanza mnamo April 22, 2013  kwa ngazi ya wataalamu na kufuatiwa na mkutano wa makatibu wakuu wa nchi wanachama na kupokea hatua zilizofikiwa katika majadiliano ya itifaki ya umoja wa fedha wa jumuiya ya Afrika ya mashariki ambao unatarajiwa kutiwa saini na wakuu wa jumuiya hiyo katika mkutano wao wa 15 mwezi Novemba mwaka huu.
Aidha mkutano huo utajadili pia pendekezo la kuongeza wigo wa mamlaka ya mahakama ya Afrika ya Mashariki kwa kupitia mapendekezo yaliojadiliwa kwenye vikao vya wataalamu na makatibu wakuu wa jumuiya hiyo.
Katika hatua nyingine mkutano huu wa dharura wa 26 wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ambao umeisha  leo kwa kuwakutanisha wataalamu na makatibu wakuu kutoka nchi wanachama wa jumuiya hiyo,  umejadili mambo matatu makuu yatakayopelekwa kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya kwa ajili ya kutia saini.
Kwa upande mwingine mkutano huu umejadili pia hatua iliyofikiwa katika uandaaji wa itifaki ya hadhi na kinga kwa watumishi wa jumuiya na taasisi zake zote.
Previous Post Next Post

Popular Items