1. Shaa
Sarah Kaisi aka Shaa ni mrembo mwenye historia ya kufanya hits tu. Tangu ashiriki shindano la kusaka vipaji la East Africa Coca Cola Pop stars, hajawahi kusimama kwa kuachia ngoma kama Shoga, Siri ya Penzi na sasa akiwa na hit mpya, Promise.
Menynah ni mshiriki wa shindano la Bongo Star Search mwaka jana na ambaye aliingia kwenye shindano hilo kwa usaili wa njia ya simu. Ni msichana mdogo ambaye baada ya shindano hilo kumalizika ameachia wimbo uitwao ‘Dream Tonight’. Pia yeye na wenzake wawili wameanzisha kundi la muziki lililo chini ya producer Lamar, Shostiz.
Mrembo huyu anafahamika pia kwa jina la Kidoti – jina ambalo limeanzisha kampuni yake ya fashion yenye jina hilo. Ni mshiriki wa Miss Tanzania, mbunifu wa mitindo, mtangazaji na msanii pia wa muziki. Hajawahi kutoa wimbo wake mwenyewe zaidi ya kushirikishwa tu. Alianza kusikika kwenye ngoma ya AY King and Queens. Mwaka jana alishirikishwa kwenye albam ya Kala Jeremiah, Pasaka na pia mwaka huu amesikika kwenye ngoma ya Lucci ‘Waters Up’ Kuna project zake kadhaa pia kwenye studio za TransformaX ambazo hazijatoka.
4. Feza Kessy
Feza Kessy ni msanii mpya aliye chini ya usimamizi wa kampuni ya AY, Unity Entertaiment. Mwezi uliopita aliachia single yake ya kwanza iitwayo Amani ya Moyo na ambayo inafanya vizuri kwa sasa. Tangu aachie wimbo wake wa kwanza, mrembo huyu aliyewahi kushikilia taji la Miss Dar City Centre amewathibitishia watanzania kuwa si kwamba kabarikiwa uzuri tu bali pia sauti tamu ya kuimba.
5. Linah
Nani asiyemfahamu Linah? Ni miongoni mwa wasanii wa kike wenye sauti tamu kuwahi kutokea Tanzania. Pamoja na Mungu kumpa sauti, amempa pia urembo unaowadatisha wanaume wengi.
Nuru Magram aka Nuru the Light ni blogger na mwanamuziki aishie Stockholm, Sweden. Pamoja na kupenda fashion, Nuru amekuwa akirudi Tanzania na kutengeneza ngoma kadhaa zikiwemo ‘Muhogo Andazi’ aliomshirikisha Bob Junior, Chapa Lapa na zingine.
7. Zuhura
Zuhuru Mrisho si msanii maarufu sana nchini licha ya kuwepo kwa muda sasa. Aliwahi kushika taji la Nokia Face of Africa 2006, lililomjumuisha kwenye ramani za mastaa wa Bongo. Mrembo huyo aliyepitia nyumba ya vipaji ya THT, alitambulishwa kwenye game ya muziki kupitia wimbo wenye jina la Limupenzi, na Shida na Raha aliyompa shavu Banana na mpaka sasa ana albam moja. Kwa sasa ana video mpya ya wimbo wake Songesha.
Baby Jay ni msanii kutoka Zanzibar ambaye mara nyingi amekuwa karibu na kundi la Offside Trick. Macho yake huwachanganya wanaume wengi.
Shilole anafahamika kama malkia wa mduara kwa sasa na amekuwa kivutio kikubwa kwenye jukwaa kila anapotumbuiza kwa jinsia anavyojua kucheza na kiuno chake. Ameshatoa hits kibao zikiwemo Lawama, Viuno Tucheze na Dudu.
Vanessa Mdee ni mrembo mwingine aliyeweka historia mwaka huu kwa kutoa single iliyoingia kwenye top ten ya nyimbo zilizopakuliwa zaidi (downloaded) mtandaoni, Closer. Pamoja na kuupata umaarufu kutokana na kazi yake ya utangazaji, mwaka huu amejipatia sifa kede kede kwa kuonyesha uwezo mkubwa katika kuimba.