SHWANGWE ZA MAFANIKIO YA BIA YA SERENGETI LAGER!

Kampeni Kabambe ya kuitangaza Bia ya SerengetiLager inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ijulikanayo kama TUPOPAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO imelitikisa mitaa na vitongoji vya jiji la Dar es Salaam jana. Huku pakiwa na
burudani ya muziki ambayo
iliashiria Shangwe za mafanikio, Msafara wa magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya
SBL pamoja na Lori kubwa aina ya Scania Semitrailer likiwa limepambwa vilivyo
na kuleta mvuto wa ajabu kwa Watanzania lilikatika mitaa mbalimbali ya jiji.
Msafara huo wa kutoa Shukrani kwa Watanzania
ndani ya jiji la Dar es Salaam ulianzia katika Kiwanda cha SBL Temeke kisha kwenda
hadi Mwembeyanga hadi Saba saba.
Shangwe hizo ziliendelea hadi Taifa, Chang’ombe,
Kamata, Msimbazi, kisha msafara huo ukaingia baranbara ya uhuru, ukapita Ilala
ukaja tokea Buguruni, ukaingia Barabara ya Mandela hadi Ubongo kisha ukapita Kituo
Kikuu cha Mabasi Ubungo, ukaelekea Sinza ukatokea Bamaga ukafuata barabara ya
Bagamoyo hadi Victoria ukaingia Mwananyamala na kumalizia viwanja vya Biafra
Kinondoni.
Aidha shsngwe hizo zilikuwa zikiendelea katika
maeneo kadhaa ya sehemu za starehe za Miti Mirefu, Kimara, Jambo park jet Lumo,
Huduma Mbagala na Airtel Pub Banana.
Magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya Serengeti yaliongoza msafara huo.

Ni mwendo wa Shangwe tu ulikuwa ukiemdxelea kila kona Gari hilo lilipopita. Mbali na kampeni hii katika Mitaa ambayo imeanzia
jijini Dar es Salaam na pia itasambaa mikoani pia Matangazo katikia vituo vya
televisheni, Redio, Magazeti na Blogs yatakuwa yanatoka pamoja na mitaani.

 Magari mengine yalikuwa Nyuma na kupambwa na chapa mbalimbali za Bidhaa za kampuni ya SBL.
Tupo Pamoja katika Shangwe za Mafanikio…

Previous Post Next Post

Popular Items