RAIS WA CHINA KUFUNGUA JENGO LA UKUMBI WA MIKUTANO LA KIMATAIFA


Xi-Jinping-China-leader1-15112012-jpg_144431 
 Rais wa ChinaXi Jinping anatarajia kufungua  jengo la ukumbi wa mikutano wa kimataifa la Julius Nyerere Convertion Centre lililopo jijini Dar -es -Salaam  linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa ziara yake nchini inayotarajiwa  kuanza mwanzoni mwa wiki ijayo.Hayo yamesemwa jana na
Katibu Mkuu  wa wizara hiyo John Haule wakati wa ziara ya kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipotembelea jengo hilo ili kuona maendeleo ya ujenzi.
 Haule alisema kuwa  ujenzi wa ukumbi huo ni matunda ya mahusiano mazuri ya ushirikiano yaliyopo baina ya  Serikali ya China na ya Tanzania kwa makubaliano maalum ikiwa ni kama msaada na mkopo nafuu usio na riba ambao utalipwa kwa awamu mbili tofauti.
 “Ukumbi huu ni wa kisasa ,utatumika  kama sekta ya utalii na biashara utasaidia kuliingizia  Taifa  fedha za kigeni kwani una  sehemu kubwa ya kuegesha magari 222, chumba cha habari,mgahawa,ofisi za wazi na maktaba ndogo”, alisema Haule.
 Aidha Haule alisema kuwa ziara ya Rais Xi Jinping ni kuimarisha mahusiano baina ya Tanzania na China  na kueneza sera ya mambo ya nje kwa kipindi chote cha utawala wake atakachokuwa madarakani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye  pia ni  mbunge wa Monduli Edward lowassa alisisitiza umuhimu wa utunzanji wa jengo hilo na kukamilisha mapema vitu ambavyo havijakamilika  ili viweze kufanyiwa kazi  kabla ya ufunguzi.
 Ujenzi wa ukumbi huo wenye ghorofa tatu na kumbi nne za mikutano  zenye uwezo  kupokea washiriki zaidi ya 1800 ulianza mwaka 2009  na umegharimu dola za kimarekani milioni 29.7.
Previous Post Next Post