NMB SASA YATOA MIKOPO YA PIKIPIKI ZA MIGUU MITATU


nmbMkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.
Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya
Fair Deal Auto Private Limited pamoja Car & General Ltd zinazosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TVS King leo zimeingia ubia wa kutoa mikopo ya pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaaj na TVS King kwa bei nafuu zaidi. Pikipiki hizi zitawawezesha wateja wa NMB kupata unafuu wa kujikimu kimaisha wakati huo huo wakiendelea na shughuli mbali mbali za kila siku.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Wajasiriamali Wadogo na wa kati, Filbert Mponzi alisema, “Mikopo hii yenye masharti nafuu kabisa, inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Mteja mwenye nia ya kupata mkopo huu atatakiwa kuwa na uwezo wa kulipia asilimia thelathini (30%) ya gharama au bei ya Bajaaj au TV’S kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi nchini yaani kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaj kwa sasa inauzwa kwa Sh. 5,450,000/= na kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TVS King Ltd inauzwa Sh. 5, 600,000/=”.
Mikopo hii ya Bajaj na TVS King kwa sasa inatolewa katika matawi tisa tu ya NMB yaliyopo jijini Dar es Salaam ambayo ni NMB Temeke, NMB Tegeta, NMB Ilala, NMB Airport, NMB Mlimani City, NMB Mwenge, NMB Mbezi, NMB Magomeni na NMB Msasani. Katika siku za usoni NMB ina mikakati ya kutoa huduma hii katika mikoa mingine ili kuwafikia wateja wengi zaidi.
Mkopo huu unaotolewa kwa muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa taratibu na makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB. Mikopo hii pia inawekewa bima inayomletea unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya asiwe na uwezo wa kufanya shughuli zake za kila siku za kimaisha au kufariki, basi bima hii itachukua jukumu la kumalizia deni la mkopo huu na mteja ataendelea kumiliki pikipiki hii ya miguu mitatu kama kawaida.
 Sasa, wateja wa NMB wanaweza kutimiza ndoto zao za kumiliki Bajaj au TVS King kwa kutumia mikopo hii. Benki ya NMB inatoa wito kwa wateja wake kutumia fursa ya kupata mikopo hii kwa unafuu zaidi na kupata fursa ya kumiliki pikipiki hizi za miguu mitatu ili kujikwamua kiuchumi.
nm2
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa Kati NMB, Filbert Mponzi (kati) Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan (Kulia) na Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja wakifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa wateja wa NMB. nm1
Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.
Previous Post Next Post