NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAISI CHARLES KITWANGA ATEMBELEA VIWANDA MKOANI MWANZA


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akionyeshwa vifaa vya kufungia samaki kabla ya kusafirishwa nje ya nchi na meneja udhibiti ubora wa kiwanda cha samaki cha Vicfish mjini Mwanza Bw Jacob Maiseli.
Naibu  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akipata Maelezo ya Utengenezaji wa Samaki na   Meneja udhibiti ubora wa kiwanda cha samaki cha Vicfish Bw Jacob Maiseli wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua Uchafuzi wa Mazingira Jijini Mwanza.
Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mbao za Plastiki Bw G Vedagiri wakiketi katika Meza iliyotengenezwa kwa Maplastiki kwenye Kiwanda cha Plastiki Jijini Mwanza Wakati wa Ziiara ya Kukadua Shughuli za Uchafuzi wa Mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akitoa Maelekezo kwa  Meneja Udhibiti Ubora Bw Jacob Maiseli kuhusu   Mfumo wa Maji taka wa Kiwanda cha Samaki cha Vicfish cha Jijini Mwanza aliofanya Ziara ya kutembelea na KujioneaUchafuzi wa Mazingira.{Picha na Ali Meja].
Evelyn Mkokoi                                    
Uelelwa mdogo kwa wananchi juu ya suala zima la uhifadhi na usimamazi wa mazingira, imeelezwa kuwa ni moja ya changamoto ya usimamiz wa mazingira katika jiji la mwanza. Hayo yameelezwa leo na Afisa Mazingira wa mkoa mwa Bw. Charles Amani wakati akiota taarifa kwa naibu wazir Ofisi ya Makamu wa Rais katika Ziara ya kutembelea viwanda mjini Mwanza.
Pamoja na changamoto hiyo mkoa pia unakabilina na upungufu wa vifaa vya udhibiti wa taka ngumu na kutokuwepo kwa teknolojia ya ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira kwa hewa kutoka viwandani na kwenye magari pamoja na kutokuwa na dampo la kisasa.
Bw. Amani maeeleza kuwa pamoja na changamoto hizo, jiji la mwanza limekuwa likiongoza kwa usafi wa mazingira kwa kipindi cha miaka saba mfululizo, kutekelezaji wa kampeni ya upandaji miti pamoja na miradi mbali mbali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Charles Kitwanga ameeleza kuwa lengo la ziara  yake mkoani Mwanza si kufungia viwanda bali ni kutaka kuwa na msimamo wa pamoja na kuzingatia  na kutekeleza sheria ya usimamizi wa mazingira, ili iwe yenye manufaa kwa watanzania, “lengo la kuja ni kuhakikisha sheria inafuatwa” alisisitiza.
Mh. Waziri aliongeza kwa kusema kusema kuwa ni vyema Halmashauri na wizara husika zikajipanga ili kuona namna ya kuwapatia sehemu mbadala wananchi wanaoishi milimani bila kuwabugudhi, ili kule nako kupangwe ili kuwe na mazingira endelevu.
Wakati huohuo, kamanda wa police wa kikosi maalum cha mazingira Nchini Bw. George Mayunga ameeleza kuwa jeshi la police lipo tayari kupambana na wahalifu wa mazingira,ili kujenga mazingira endelevu.

Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA