Na: Denis Gasper, Iringa
TIMU ya Mshindo Fc ya Iringa imeibuka mabingwa wa Kombe la Mwakalebela baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 37 na kuwazidi kete waliozoa pointi 35 timu ya Magereza Iringa iliyoshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu imekwenda kwa Mtwivila City mechi zilizoendeshwa kwa mtindo wa ligi. Ubingwa huo umeiwezesha timu ya
Mshindo kuondoka na kitita cha shilingi laki 5 na washindi wa pili ambao ni Magereza wamejinyakulia kiasi cha shilingi laki 3 wakati timu ya Mtwivila City wamekamata nafasi ya tatu na kuondoka na kiasi cha shilingi laki 1 fedha ambazo watakabidhiwa rasmi leo(Jumamosi) na mdhamini mkuu wa mashindano hayo Fredrick Mwakalebela katika uwanja wa Samora.
Ligi hiyo iliyoanza Novemba11 mwaka jana na kuhusisha timu zaidi ya kumi ilikuwa na zawadi kwa mfungaji bora kiasi cha shilingi laki 1 na zawadi hiyo imeweza kwenda kwa Kassimu Mataka na David Muhanga, Timu yenye nidhamu imechukuliwa na Uhuru Fc nakuzoa kitita cha shilingi laki 1.
Ligi hiyo imegharimu jumla ya shilingi milioni 2.7 zilitumika katika kugharimia vifaa kama vile jezi jozi 6 za waamuzi, mipira 10, nyavu za viwanjani pamoja na gharama za uendeshaji wa mashindano, zikiwemo zawadi.