MAFUTA YA ALZETI YABAINIKA NI TIBA MBADALA KWA MAGONJWA YA KANSA ,TB,PRESHA NA VIDONDA VYA TUMBO


Mafuta  ya kula yatokanayo na zao la Alizeti linalopatikana kwa wingi mkoani Singida, yamebainika kuwa dawa muhimu na mbadala ya kukabiliana na maradhi ambayo wataalamu wa tiba za kisasa wanayaita ni sugu.
Habari za uhakika zilizopatikana mjini Singida, zimesema kuwa tayari baadhi ya makampuni makubwa ya ndani yaliyoanza kununua zao hilo kinyemela, yalipata soko kwa baadhi ya nchi za mashariki ya mbali na kujinufaisha bila wadau husika kujua.
Mbali na mkoa wa Singida, zao hilo pia hulimwa kwa uchache katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Shinyanga, Iringa na Ruvuma, na hii ni kulingana na takwimu zilizopo katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Tayari kuliibuka mvutano mjini Dodoma ambako kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka jana lilikuwa likinaendelea kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Paseko Konne, aliyekuwa akilalamikiwa na baadhi ya wabunge wa mkoa huo kuhusu suala hilo.
Konne alidaiwa kutoa zuio kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kuzunguka vijiji kununua zao hilo kwa hatua za ulaghai kwani hatua hiyo inaweza kumkosesha haki ya kujua hali ya soko la siku mkulima.
Aidha, alitaka kama utaratibu huo utaonekana kuwa na athari zaidi na kwa nia ya kuongeza ari ya kilimo, wakulima wa zao hilo washauriwe kuuza mazao hayo kwenye vyama vya ushirika vya msingi kwenye vijiji, kata au Tarafa zao.
Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, mtafiti mmoja wa tiba za asili Mkoani Singida Dk. Raelk Mhlinyo, amesema amekuwa akitumia mafuta ya alizeti kwa ajili ya kutibia watu magonjwa mbalimbali yanayowakabili.
Lakini pia Dk. Mhlinyo amesema mkoa huo wa Singida, umekuwa ukipokea wageni kutoka mikoa mingine ya kanda ya ziwa, wanaokwenda kununua mafuta ya alizeti kwa ajili ya kupeleka kwenye maeneo yao kwa ajili ya tiba.
“Mimi nina imani kubwa, hata vita zinazoendelea katika suala hili ni kwa wadau kutambua ndani ya alizeti kuna nini zaidi ya kupata mafuta kwa ajili ya kupikia kwenye chakula,” amesema Dk. Mhlinyo.
Dk. Mhlinyo ameongeza kusema kuwa alipata utaalam na elimu kuhusu matumizi ya mafuta ya alizeti kama dawa ya kutibu maradhi ya binadamu kutoka kwa mtaalam wa tiba za asili nchini Botswana Dk. Banaye Mwililowe.
“Huyu jamaa alikuja Tanzania mwaka ya 1998 kwenye maonyesho na aliona nikihangaika kushawishi watu kununua dawa zangu, ambazo kwa wakati huo hata sikubahatika kusogelewa kirahisi,” amesema Dk. Mhlinyo.
Alifafanua baada ya kuanza mazungumzo, Mwililowe alimpa moyo na kumtaka kuongeza jitihada zaidi na hasa katika kuwasaidia watu kama huduma badala ya kutaka kupata faida ya haraka.
“Kwa hiyo alinisaidia sana, nami kwa kutaka kujua zaidi nilifanya safari mpaka Zambia, ambako Mwililowe amefungua ofisi eneo la Ndora, na kukutana naye, hivyo tulifanya safari mpaka Botswana ambako nilimsaidia kazi kwa kipindi cha miezi mitano,” amesema.
Amesema alifanikiwa kubaini mafiuta ya alizeti kuwa ni dawa muhimu kwa maradhi yanayozumbua maisha ya watu wengi na hasa wenye umri mkubwa, hivyo aliondoka huko na kurejresha nchini akiwa amenufaika.
Dk. Mhlinyo amesema mafuta hayo huchanganywa na dawa mbili za miti shamba kwa ajili ya kutibu magonjwa kama TB, Kansa ya Damu, Vidonda vya Tumbo na Shinikizo la Damu, kwa jamii na kusema hatua hiyo inaendelea kusaidia zaidi watu wenye matatizo.
“Ninatibia watu hapa, na mafuta ya alizeti ni moja kati ya viungo dawa muhimu kwa kazi hii, ninayapenda sana kwa vile yameendelea kusaidia wagonjwa na kutokana na hali hiyo nimelazimika kulima hekari kadhaa ili kuwa na malengo zaidi,” amesema Dk. Mhlinyo.
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Tiba Asili katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Paul Mhame, alipoulizwa kuhusu uwezekano wa mafuta hayo yenye virutubisho muhimu vya asili kuweza kutibu magonjwa ya aina hiyo, alisema ‘hakuna ubishi hilo linawezekana kabisa’.
“Ninachoweza kusema hapa ni kwamba miti shamba ni miti dawa, na kutokana na hali hiyo, mafuta yeyote yatokanayo na mazao ya asili na yasiyo na mchanganyiko wa kemikali, yanaweza kuwa dawa muhimu za kutibu na wala sio kutuliza maradhi hayo,” alisema Dk. Mhame.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisisitiza dawa hizo pamoja na kuwa ni utafiti wa kijadi na asili zifikishwe kwenye mamlaka husika ziweze kufanyiwa uchunguzi wa kina na kupewa kibali.
Baadhi ya madaktari waliozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu suala la mafuta hayo, wameonyesha kuunga mkono kauli ya Dk. Mhlinyo, wakisema kuna kasi ya kupungua kwa idadi ya watu wanaohitaji matibabu kwa baadhi ya maradhi.
“Inawekana kabisa, matumizi ya mafuta haya kipekee pamoja na huo mchanganyiko wa dawa zake unaweza kusaidia kutibu maradhi mengi na ndio maana idadi ya wahitaji wa huduma za afya kwa mikoa ya Tabora, Singira na Shinyanga imepungua,” alisema Dk. Jumanne Abdallah wa Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Mtaalam huyo alisema utafiti zaidi unapaswa kufanyika ili kubaini maradhi mengine yanayoweza kutibika kwa kutumia ushauri wa kubadili mfumo wa mafuta na vyakula bila dawa, na kusema jitihada za makusudi zinapaswa kuchukuliwa kwa ajili ya kusaidia jamii.
Dk. Mhame hata hivyo, aliwashauri viongozi wa serikali ngazi za wilaya na mikoa, kuhamasisha wananchi kilimo cha zao hilo kwa nia ya kuimarisha hali zao kiuchumi, kwa maana ya kujiongezea kipato na kukabiliana na hali duni ya maisha na umasikini.

Previous Post Next Post