KIFURUSHI CHA ZIADA CHA TIGO KWENYE HUDUMA ZA BLACKBERRY

Kifurushi  cha Blackberry  cha Tigo kimewapa wateja wao  fursa yakuweza kutumia mitandao ya kijamii kwa bei nafuu zaidi kijulikanacho kama Blackberry Social Plan.
Kifurushi hiki kimewawezesha wateja wa Tigo kutumia mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook, Whatsaap na mingineyo  ipasavyo kwa gharama nafuu zaidi. Watumiaji wanaweza kujiunga na kifurushi cha siku, wiki au mwezi kutokana  na matumizi yao.
Kutumia huduma hii mteja inabidi ajiunge kwa kutuma ujumbe kwenda 15518 wenye neno BBS1 kutumia kifurushi cha siku, BBS7 kutumia kifurushi cha wiki, na BBS30 kutumia kifurushi cha mwezi.  Gharama za siku ni shilingi 499, za wiki shilingi 2,999 na za mwezi shilingi 11,999. 

Previous Post Next Post