LEMA ATOA WARAKA WAKE KWA RAISI KIKWETE


Mbunge wa Arusha Mjini  Godbless Lema akionyesha CD uliojaa waraka wa Rais Kikwete
WAKATI  mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na kufanyiwa dua kwani wewe ndie unatumikia ofisi kubwa kuliko zote Nchini na wakati huo huo unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo ya kutumikia ofisi kubwa na ya Heshima kuliko zote Nchini.
Nimekuwa nikitafakari sana suala la Udini katika Taifa letu na huko nyuma mwaka jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua mathubuti kabla mambo hayajaaribika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa ambao siku hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma.
Nape na wenzake pia walipata fursa ya kuusoma,Mh Rais katika waraka hule nilisema hivi “ Mh Rais Taifa linahitaji Tiba “ siwezi leo kuandika kile nilichosema katika waraka ule ila niliweza kubashiri sumu ya udini inayoendelea katika Taifa lako na langu, Mh Rais , ukweli nakwambia ukifanya mchezo kidogo sana Taifa hili linapotea likiwa mikononi mwako kwani hali ya nchi sio nzuri hata kidogo na watu waliokuwa wanaishi kwa umoja na upendo sasa wanaanza kutafuta mbinu za kugombana na kuuwana.
Mh Rais, Siasa ya Udini na Ukanda makusudi yake yalikuwa kudhoofisha vyama vya upinzani na yalifanikiwa kwa baadhi ya vyama kudhoofishwa sana na mkakati huo unaendelea dhidi ya Chadema lakini kinachosikitisha ni kuwa wale waliobuni mkakati huo walishindwa kutafakari au kuona madhara yake mbele .
Mh Rais, mkakati wa kudhoofisha Chama cha Siasa kwa Udini na Ukanda hauishi tu kuangamiza hicho Chama bali kuwagawa Watu na Taifa kwa Ujumla , Mtu anapojaribu kusema Chadema ni Chama cha Wakristo kimsingi matamshi hayo hayaangamizi Chadema tu bali yanagawa Watu kwa matabaka ya Udini wao na kufanya Dini moja iamini kuwa Dini nyingine ni mbaya na hivyo mpango huo unafanya Watu waanze kutazamana kwa Udini na Ukabila na matokeo yake ndiyo haya tunaanza kuyaona leo .
Mh Rais, Taifa linahitaji tiba , Hivi karibuni Waziri Mkuu alienda Geita kwenye mgogoro wa Waisilamu na Wakristo na niliona mawazo ya Waziri Mkuu kwenye vyombo vya habari na kwa kweli nilisikitika kwa busara zile zilizokuwa zimejaa hofu kubwa . Tatizo lile lilianza na nani kati ya Mkristo na Muislamu anayepaswa kuchinja?.
Previous Post Next Post