President Jakaya Kikwete amesema Serikali itaendelea kuboresha utoaji wa mikopo kwa Wanafunzi ambapo kwa mwaka huu wa fedha, zimetengwa bilioni 345 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi elfu 98 na mia 772 wa elimu ya juu kote Tanzania.
Hii kauli ameitoa akiwa Morogoro kwenye uzinduzi wa jengo kwenye chuo kikuu cha Kiislamu ambapo kwenye sentensi nyingine, President alisema mikopo iliyotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2005 ni bilioni 56 na kusisitiza kwamba bodi ya mikopo Tanzania inatakiwa kufatilia wahitimu wa vyuo vikuu walipe deni ili wengine wasaidiwe.