Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba kukutana na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume, Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam, Leo (Alhamisi, Machi 7, 2013) kuanzia saa 4:00 asubuhi. Katika mkutano huo, Jaji Warioba atazungumzia uundwaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Waandishi wa Habari wa vyombo vyote mnakaribishwa