Japo mpaka sasa sijapata kauli ya jeshi la Polisi kuhusu askari wa kike wa usalama barabarani aliegongwa na gari na kufariki march 18 2013, kuna ripoti nimeipata kutoka kwa mashuhuda.
Ajali imetokea Bamaga Dar es salaam muda mfupi tu baada ya msafara wa Rais kupita ambapo gari linalodaiwa kumgonga halikuwa sehemu ya msafari wa Rais.
Kuna kawaida ya madereva hasa wa Dar es salaam huvizia na kupita nyuma ya msafara wowote kwa sababu ya kukwepa foleni, sasa gari lililomgonga askari huyu nalo lilikua limejiunganishia kwenye msafari ili kukwepa foleni.
Mashuhuda wanasema “askari huyu kabla ya kugongwa asubuhi yake alimsaidia kwa kumpeleka hospitali mtu mmoja ambae aligongwa kwenye eneo hilohilo na kujeruhiwa mbavu ambapo saa kadhaa baadae ndio yeye akagongwa na kufariki, askari aliekimbiza hilo gari lililokimbia baada ya kugonga alithibitisha kwamba wamelikamata pamoja na dereva”
Chanzo cha ajali ni baada ya msafara wa rais kupita ambapo askari huyo alisimamisha magari ya kutoka Sayansi kwenda Mwenge na kuanza kuruhusu magari yanayotoka Shekilango kwenda Sayansi ambapo kulikua kuna gari jingine lililoachwa kwa mbali kidogo na msafara lilikua spidi wakati tayari wakati huo Marehemu alikua ameanza kuruhusu magari yatoke Shekilango kwenda Sayansi, baada ya hapo dereva aliemgonga akapita kwa kasi na kumgonga trafiki huyu ambae alichanganyikiwa na kuinama kisha gari likamgonga na kuendelea na safari, pamoja na spidi kubwa ya gari.. dereva alimudu na halikuweza kupinduka kisha akaendelea kukimbia”
Bado naendelea kusubiri kufahamu polisi watasema nini leo manake hawajatoa taarifa bado…..