HAYA NDIYO ULIYOKUWA HUYAFAHAMU KUMHUSU PAPA FRANCIS HAYA HAPA

Pope Francis I
Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina ndiye papa ambaaye anachukua nafasi ya Benedict XVI, na baada ya kupita kama papa katika uchaguzi amechagulia jina la Papa Francis I. Haya ni baadhi ya mambo ya muhimu kumhusu.

*Ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.

*Ni mzaliwa wa Buenos Aires huko Argentina mwaka 1936.

*Ni muitaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la Usafiri wa Treni kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.

*Kadinali Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina.

*Ana umri wa mwaka 76, na kwa miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina.

*Inasemekana kuwa yeye ndiye aliyeibuka nambari mbili katika uchaguzi wa Papa mwaka 2005 Papa Benedict XVI aliposhinda.

Moshi mweupe ulioashiria Papa amepatikana

*Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema utamsaidia sana katika uongozi wake.

*Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.

*Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina pamoja na kushikilia misingi.

Pope Francis I akiongea na waumini mara baada ya kuchaguliwa
Previous Post Next Post