Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt.Terezya Huvisa akiwa hutubia Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni Wakati Sherehe za Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Sherehe hizo zimefanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es Salaam leo.
Mawaziri wa Nchi Katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan na Wa mazingira Dkt. Terezya Huvisa, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Chalers Kitwanga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Sar es Salaam Said Meck Sadiki wakifanya Usafi Kandokando Mwabarabara ya Kawe Wakati wa Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika Sherehe hizo zimefanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meek Sadiki akifanya Usafi Wa jiji katika Barabara ya Kawe kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Wakati wa Kuadhimisha Siku ya Mazingira Barani Afrika. Kulia Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Julius Ningu.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Wakifanya Usafi Kuadhimisha siku ya Mazingira Barani Afrika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.[Picha na Jr Botea].



