AFRICAN BARRICK GOLD KUONGEZA UWEKEZAJI WA MFUKO WAKE WA MAENDELEO WA ABGT


1
 Greg Hawkins, Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza mpango wa maendeleo wa kampuni hiyo kwa wananchi wanaozunguka mgodi wa Africa  Barrick Gold Mine leo.
2 Baadhi ya maofisa kutoka kampuni ya kuchimba madini ya Africa Barrick Gold Mine wakiwa katika mkutano huo leo 9
 Greg Hawkins, Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG  akijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya Hyatt Regency leo, kulia ni Deo Mwanyika Vice President Corporat Affairs wa kampuni hiyo na katikati ni Steven Kisakye Meneja Mawasiliano.
……………………………………………………………………………………
• Zaidi ya miradi 50 yapatafa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo wa kampuni ya ABG
• ABG yasisitiza kuendelea kuwekeza dola za Marekani milioni 10 kwenye mfuko
 Kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold (ABG) inafuraha kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo wa ABG tangu kuanzishwa kwake mnamo Septemba 2011.
 Mfuko huu umesimamia uwekezaji wa kampuni ya ABG kwenye jamii katika kipindi kilichopita cha miezi 18 na kufanikiwa kutekeleza zaidi ya miradi 50 yenye thamani ya dola za Marekani milioni 7.5 (takriban shilingi bilioni 12 katika kipindi cha mwaka 2011/12.
 Greg Hawkins, Afisa Mtendaji Mkuu wa ABG, amesema: “Tunafurahi kuona mafanikio makubwa ambayo Mfuko wa Maendeleo wa ABG umeyapata kwenye kipindi cha miezi 18 mpaka sasa. Tulianzisha Mfuko huu kama sehemu ya jitihada zetu za kuchangia kwenye maendeleo endelevu nchini Tanzania na tayari tumeona mafanikio makubwa kwenye zaidi ya miradi 50 mpaka sasa.”
 ”Tunaendelea kuweka msisitizo kuhakikisha kuwa jamii zinazotuzunguka zinapata faida kutokana na kuwepo wa shughuli zetu kwenye maeneo yao na ninafurahi kutangaza kuwa kampuni ya ABG itaendelea kutenga dola za Marekani milioni 10 kila mwaka kwa ajili ya uwekezaji wa Mfuko wa Maendeleo wa ABG kwa mwaka 2013.”
 Mpaka hii leo, Mfuko wa Maendeleo wa ABG umewekeza dola za Marekani milioni 2.2 (zaidi ya shilingi bilioni 3.6) kusaidia kuboresha afya ya umma kwenye jamii zinazozunguko migodi yake.
Previous Post Next Post