Takriban wateja 11 wa Mtandao wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, wameibuka washindi wa promosheni ya ‘sms mega promo’ inayoendelea nchi nzima na kujinyakulia jumla ya kitita cha pesa zaidi ya Sh18milioni.
Washindi hao walipatikana katika droo kubwa ya promosheni hiyo iliyofanyika hivi karibuni Dar es salaam, ambapo washindi 9 walijinyakulia jumla ya Sh1 milioni moja kila mmoja wakati wengine wawili wamejishindia Sh5milioni kila mmoja.
Wateja wawili kwa wiki hii walioibuka washindi kwa kujipatia Sh5 milioni kila mmoja ni pamoja na mfanyabiashara, mkazi wa Mbeya, Joel Stuart (24), na Baraka Mtasigwa (24) kutoka Mtwara,anayejishughulisha na uuzaji wa samani.
Waliojishindia Sh1 milioni moja kila mmoja kwa siku tatu mfululizo toka kuanza kwa kampeni hiyo takribani siku tatu zilizopita, na mikoa wanayotoka katika mabano ni pamoja na Rayness Benjamini (Arusha), David Damian (Shinyanga), Aristides Ndole (Tanga).Wengine ni Ruth Mungule (DSM), Agasese Joseph (Dsm), Benjamin Mbawala (Songea), Steven Chapire (Arusha), Jane Mary Mosarito (Rukwa) na Besti Monyo (DSM-Mabibo).
Mkuu wa Kitengo cha Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, alisema promosheni hiyo itasaidia kuboresha maisha ya kila mmoja.
ya aina yake inatoa fursa kwa wateja wa Vodacom kujishindia hadi Sh milioni 5.
“Nawasihi wateja wetu jitokezeni kushiriki katika promosheni hii ya aina yake na ambayo inatoa fursa ya kubadili maisha ya kila mmoja wetu bila kutarajia, nafasi ni hii kwa yeyote kuweza kujishindia” alisema Twissa.
Jumla ya Sh438milioni zinaendelea kushindaniwa ndani ya siku 90 nchi nzima,na wateja wote watakaoibuka washindi watajulishwa kwa njia ya simu sambamba na kupewa utaratibu maalumu wa kuchukua fedha zao zitakazotolewa kwa njia ya M-Pesa.
Alifafanua kuwa kupitia kampeni hiyo,wateja watatu watakaoshinda kwa kujibu maswali vizuri waliyoulizwa kupitia ujumbe mfupi wa maneno watajinyakulia Sh1milioni kila mmoja kila siku. Wakati wengine wawili watakaojibu vizuri zaidi watajipatia hadi Sh5milioni kila mmoja ndani ya siku saba.