Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa wanafanya usafi pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala Muheshimiwa Jerry Silaa.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika picha ya Pamoja na Muheshimiwa Meya wa Ilala Jerry Silaa.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa wanafurahia baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi katika Fukwe ya Bahari ya Hindi leo.
Washiriki 40 wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka mikoa yote na vyuo vikuu waliopo katika kambi ya Taifa Ikondolelo Lodge wakijiandaa na fainali za Taifa zitakazofanyika Tarehe 16.02.2013 Dar Live Mbagala. Wameshiriki katika zoezi la kusafisha ufukwe wa Bahari pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala Muheshimiwa Jerry Slaa.
Tamasha hilo maalum la kutunza na kujali Mazingira pamoja kuonesha umuhimu wa mazingira liliandaliwa na Shirika la Nipe Fagio ambalo limejikita katika mambo kusaidia jamii pamoja na Mazingira.
Katika Tamasha hilo ambapo Viongozi mbalimbali wa Serikali, pamoja na wananchi mbalimbali walihudhuria na kufanya usafi huo kuanzia saa moja asubuhi mpaka sa nne kamili asubuhi siku ya Jumapili, zoezi lilienda vizuri ambapo Warembo wa Miss Utalii Tanzania walishiriki kikamilifu na walionesha mfano mzuri kwa kuchapa kazi zaidi ya kukusanya taka taka hizo.