
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Mh. Jerry Silaa akizungumza na wananchi wa Kata yake ya Gongo la Mboto ambapo amewasihi viongozi wa CCM ngazi za Chini kuhakikisha wanafuatilia na kutafutia ufumbuzi kero zinazo wakabili watu wanaowazunguka
.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi na wana CCM kwa ujumla kufuatia kuteuliwa na Mh.rais kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na kusema ofisi za chama zinatakiwa kuwa wazi kuanzia ngazi ya kata mpaka mkoa ili wananchi waweze kufika kutoa kero zao.
Aidha amewataka viongozi wenzake kufanyakazi kwa ushirikiano na uadilifu, na kuwa wale viongozi wachache wasio waadilifu watashughulikiwa kikamilifu ili kuleta ufanisi ndani ya chama.

Mmoja wachekeshaji katika mikutano ya CCM wanaofahamika kama Aki na Ukwa akimwombea Dua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kuzungumza na wana CCM wa Gongo la Mboto.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na wananchi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.

Baadhi ya kinamama wa Gongo la Mboto ambao ni wananchama wa CCM wakiwasili kwenye Uwanja uliopo karibu na reli Gongo la Mboto katika mkutano wa hadhara wa kumpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na waendesha Boda boda wa Gongo la Mboto waliofika kumlaki akitokea mjini Dodoma.