WAASI WA NCHINI MALI WAUA MWANAJESHI MWINGINE WA UFARANSA


Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imesema mwanajeshi wa Ufaransa ameuawa katika mapigano makali na wanamgambo kaskazini mwa Mali, na takribani waasi 20 wa kiislamu wenye itikadi kali wameuawa katika mapambano hayo.

Vifo hivyo vimetokea wakati wa operesheni ya vikosi maalum katika eneo la milima la Adrar des Ifoghas na kufanya idadi idadi ya wanajeshi wa Ufaransa waliouawa tangu kuanza operesheni ya Ufaransa nchini Mali mnamo Januari 11 kufikia wawili.

 Ufaransa imesema shambulizi hilo la karibuni linalenga kuyavuruga makundi ya kigaidi katika eneo ambalo wanaaminika kuchukua hifadhi.

Previous Post Next Post