Mwenyekiti wa kamati ya TWAA Bi Sadaka Gandi akiongea na Waandishi wa Habari Leo
----
DAR ES SALAAM, TANZANIA, – Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) imezindua Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka 2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya jamii zao kwa njia moja au nyingine.
"TWAA inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao wameweza kupata mafanikio makubwa sit u kibinasi bali wametumia nafasi zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya kwanza mafanikio na michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la kufajiri na kuridhisha sana.”
Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali, Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Sayansi na Teknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko Mdogo.
Bi Sadaka Gandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteua wanawake wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili wa tuzo hizi huko nje ambao ni mawakala wa mabadiliko katika jamii zao. Tunataka kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko. Kamati ilipokea fomu za nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "
Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi - Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello - Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dk Marcelina Chijoriga- Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi. Ludovicka Tarimo – Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi - Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia - Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli. Huko nyuma tuzo hizi zilidhaminiwa na Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, Watu wa Marekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA, UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement, Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.
KUHUSU TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA)
TWA ni taasisi isiyo ya kiserikali, ya hiari na kujitegemea inayojihusisha na uwezeshaji wa wanawake iliyoanzishwa mwaka 2009. Lengo kuu la TWA ni kuimarisha ushiriki, na majukumu ya wanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mabo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. TWA inafanya kampeni, mafunzo, semina, mikutano na warsha ambazo zinakuza ubadilishanaji wa taarifa na ushauri kwa wanawake na wasichana wadogo wa Kitanzania.
Kampeni na mafunzo haya yanalenga zaidi haki za binadamu na za wanawake, usawa wa kijinsia, ushiriki wa wanawake kweye shughuli za kiuchumi na kijamii.Kazi kubwa ya TWA ni kuboresha maisha, kupanua fursa, na kuwasaidia wanawake katika Tanzania kushamiri na kuchangia kwenye ustawi wa nchi. TWA inafanya kazi na viongozi ,watu binafsi, jamii, mashirika yasiyo ya kiserekali, serikali, sekta binafsi na wafadhili wa nje kujenga ufanisi na kuhakikisha malengo ya kuendeleza wanawake yanafanikiwa. Sisi ni kosa kwa maendeleo ya Tanzania kuendelea mpaka kila mwanamke anakuwa mabadiliko. Tumejikita kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea na wanawake ni chachu ya maendeleo hayo.