REAL vs MAN U HAKUNA MBABE, MASHABIKI WA DARTMUND WAFA KWA AJALI.

Katika mechi baina ya Rael Madrid na Manchester United vigogo hao wa soka waliishia sare ya bao 1-1 kwenye dimba la Bernabea . Kama ilivyo kwa Dortmund, Man U nayo imejiweka katika nafasi nzuri ya kuinusa robo fainali.

 Cristiano Ronaldo aliifungia Real bao la pekee katika mchezo huo. Man U walicharuka na kufanya mambo pale mpira wa kona uliopigwa na Wayne Rooney kufika miguuni mwa Danny Welbeck ambaye hakufanya ajizi na kuuweka kimyani mnamo dakika ya 20.

 Ronaldo alisema kuwa wangelikuwa na nafasi tena dhidi ya Man U katika mchezo wa marudiano Old Trafford lakini ndo hivyo mambo hayakuwa mazuri. Kocha wa Manchester Sie Alex Ferguson aliuelezea mchezo huo kuwa ulikuwa mgumu na kukiri kuwa Real ni timu imara lakini akaongeza kuwa walicheza vizuri na walistahiki kupata mabao zaidi ya hilo moja.

Nao mchezo baina ya Dortmund dhidi ya Shakhtar Donetsk ulimalizika kwa bao 2-2. Mlinzi wa Dortmund Mats Hammel ndiye aliyefanya mambo kuwa mazuri kwa timu yake baada ya kuitumia vizuri kona iliyopatikana dakika tatu kabla ya kupulizwa kipenga cha mwisho katika mchezo huo.

 Hata hivyo huko Donetsk licha ya Dortmund kupata nafasi nzuri lakini mchezo huo uliingia dosari kutokana na vifo vya mashabiki watano wa kandanda walifariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya ndege aliyokuwa wamepanda kutoka Odessa kusini mwa Ukraine iliyokuwa imebeba watu 45 ilipopata ajali wakati wa kutua katika uwanja wa ndege wa Donetsk.

 Ajali hiyo ilitokea muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya Dortmund na Shakhtar na inaaminika kuwa wengi wa watu hao walikuwa ni mashabiki wa kandanda waliokuja mjini humo kushuhudia mechi hiyo. Kabla ya kuanza kwa mchezo timu zote mbili zilisimama kwa dakika moja kuwaombea marehemu.

 

Previous Post Next Post

Popular Items

Music: Nikki Mbishi - Utamwambia nini

Magazetini Leo Ijumaa ya Tarehe 20/9/2013