Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na maafisa mbalimbali wa ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa jana jioni ya Februari 24, 2013 baada ya kuhudhuria hafla ya Utiaji saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Rais Kikwete, kabla ya kurejea Dar es salaam leo, alikwenda Uganda kuhudhuria mazishi ya baba mzazi wa Rais Yoweri Kaguta Museveni, Mzee Amos Kaguta, aliyefariki siku ya Ijumaa na kuzikwa kijijini kwake
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Profesa Joram M. Biswaro akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Balozi Naimi Aziz (kati) na Afisa ubalozi Samwel Shelukindo wakipungia kumuaga Rais Kikwete wakati ndege yake ikiondoka uwanjani hapo jana jioni ya Februari 24, 2013.Picha na IKULU