ARFI ATAHADHARISHA CCM KUGAWA WANANCHI



Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa Said Arfi, akihutumia katika mkutano wa hadhara  wa Dodoma kwenye Viwanja vya Mwanga Bar na kuhudhuliwa na umati wa watu.

Na Bryceson Mathias-Dodoma.
 MAKAMU Mwenyekiti wa chama cha Demokrasi  na Maendeleo Taifa na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi, amewataka watanzania kamwe wasikubali kugawanywa, kudanganywa, kutenganishwa na kukosanishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kinachopandikiza itikadi za udini.

Arfi alisema hayo katika Mkutano wa adhara uliofanyika katika Viwanja vya Mwanga Bar mkoani Dodoma Akihutubia maelfu ya watu ambao baadaye walijipanga na kuwapa kadi za Chadema baada ya kuamua kuvua Magamba na kuvaa Magwanda  Arfi alisema, awali CCM walitumia njia hiyo kwa kukiita Chama cha wanachi CUF ni cha Ki-Islam na wakafanikiwa kukisambaratisha kwa Wakristo kukihama.
 “Baada ya Mbinu za kukiita Chadema ni kikabila na kwamba ni cha Kikristo kushindwa, sasa wameanza kutafuta Mbinu za kuwapotosha, kuwadanganya, ili  kuwatenganisha,  kuwakosanisha, kuwaogofya,  kuwatishia na kuwapandikizia udini”.alisema Arfi akisema yeye ni M-Islamu na hajawahi kupata hasara.
 Huku akishangiliwa na uwanja mzima Arfi alisema, yeye ni M-Islamu, hakuna mahali ndani ya Kurani panaposema mtu aue halafu Mungu atampa kheri na pepo, akiwa Ahera zaidi ya Laana kumuanzia hapa duniani.
 Aliwashukia Polisi na Usalama wa Taifa kuwa ifike mahali wasione aibu kusema wameshindwa wajibu wao wa kuwalinda watanzania, jamboa alilosema kama wameshindwa, sasa wanatakiwa wakae pembeni na wakikaidi  watalazimishwashwa na guvu ya Umma.
Mbali ya shutuma hizo Arfi aliitaka Serikali ya CCM iwaombe radhi watanzania kwa kuwaigiza kwenye ugomvi wa kidini, ambapo hapo awali alisema hakuna mtu aliekuwa akiuliza habari ya kuchinja na kugombea madarakani kwa Udini, Ukabila, Undugu, Urafiki na Upenzi.
Arfi aliiponda CCM na Viongozi wake akisema, hivi sasa wanatumika kupoteza fedha za walalhoi mamilioni kwa mamilioni  kupigia kura ya maajabu ya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti, badala ya kutumia fedha hiyo kukomesha maajabu ya mtoto kufaulu mtihani kwenda Sekondari wakati hajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
Aidha aliwasihi watanzania wajiulize mioyoni mwao, Je kura yao imewasaidia nini? Kama haijawasaidia basi kwa mtu yeyote waliyempa madaraka na wajibu huo, basi waihukumu Serikali hiyo mwaka 2015 na kudai hilo litawezekana tu kwa kuunganisha nguvu na kuing’oa CCM madarakani.
Awali Kigaila akiwahutubia wana Dodoma kabla ya kumuachia Uwanja Arfi alisema, Kitendo cha Spika wa Bunge Anne Makinda kuzima Hoja za Wapinzani ya James Mbatia kuhusu Udhaifu wa Sekta ya Elimu yenye Maslahi kwa Watanzania na ya John Mnyika kuhusu Shida ya Majiji Jijini Dar es Salaam na nchi nzima, ingekuwa ni Arusha asingeingia bungeni wananchi wangemzuia kwa nguvu ya umma.
Huku akishangazwa na uoga wa wananchi hao, Kigaila aliwashukia akisema, wakazi wa Dodoma ikifika hapo ndipo mahali huwa wanauza utu na kupoteza haki yao ambapo watu hurudi nyuma na kujificha kwenye uchochoro wa nyumba na Mitaa yao wakajifungia ndani.
Kigaila alisema lakini siyo watu wa Arusha.  Arusha, Waziri Shukuru Kawambwa na Naibu wake Philip Mulugo wasingethubutu kunusa bungeni  waje wawahadai wananachi kutokana na kuwaharibia watoto wao kwa Elimu yao feki, huku wakiwasomesha watoto wao ulaya ili waje wawatawale wa walalahoi.
Mapema Kigaila aliwataka usalama wa taifa waweke vyombo vyao vizuri ili wamfikishie habari na Salamu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi, sababu za kuzuia mikutano wakati wa Bunge ambapo aliwahoji wananchi akisema,“Huyu Mama Dk. Nchimbi ana Muda gani hapa Dodoma?..watu; .muda mfupi …tu... miaka yote  Bunge lilikuwa linafanyika au halifanyiki! Linafanyika!! Je mikutano ilikuwa haifanyika?...inafanyika!! kauli hizi zinatokana na watu wasio na kazi za kufanya ndiyo maana Chadema kinasema kwenye Katiba hakitaki Mkuu wa Mkoa, Wilaya, Waziri  awe Mbunge, Jaji na Spika wa kuteuliwa na Rais, vinginevyo tutaikataa”.
Previous Post Next Post