Hali ya usafi katika uwanja wetu wa taifa sio nzuri na inatia kinyaa kwa kweli pia ni aibu kwa soka letu na nchi kiujumla.
Katika mchezo wa Jumatano kati ya Tanzania na Cameroon katika jukwaa la VIP C nilishuhudia kinyesi cha binadamu kikiwa kimezagaa katika ngazi za kwenye siti za uwanja huo.
Kutokana na kuona uchafu huo ikabidi nianze kufuatilia suala hilo kwanini kinyesi kile kipo pale, katika kuuliza kwangu nikagundua kwamba baadhi ya vyoo vilikuwa vimejaa na kutapika hivyo inawezekana kuna shabiki mmoja wapo aliyekosa ustaarabu aliamua kujisaidia kwenye eneo hilo baada ya kubanwa na haja.
Lakini uwanja huu wa taifa umetoka kuchezewa mechi mbili kubwa wikiendi iliyopita na katika mechi hiyo tuliambiwa kwamba kuna mamilioni yalikuwa yamekatwa, katika mechi ya Yanga na Mtibwa zilikatwa shilingi millioni15,435,255.48, wakati kwenye mechi ya Simba vs JKT zilikatwa
8,869,704.64, hivyo ndani ya siku mbili uwanja ulichukua zaidi ya Millioni 24.
8,869,704.64, hivyo ndani ya siku mbili uwanja ulichukua zaidi ya Millioni 24.
Sasa kweli kihulasia ni wapi fedha hizo zinakwenda kiasi cha kushindwa hata kutoa fedha za kusafisha uwanja pamoja na kuvuta vyoo au kurekebisha hali iliyopo vyooni ili kuepeuka uchafu unaokuwepo uwanjani?
Tunatia aibu kwa jambo hili na pia tunahatarisha afya za mashabiki wanaoingia uwanjani kuangalia mechi.