Mfuko wa hifadhi ya jamii hapa nchini(NSSF)umesema kuwa kwa sasa unaandaa mpango maalumu ambao utalenga kuondokana na Umaskini wa Nchi ya Tanzania huku mpango huo pia ukiongeza ufanisi wa masuala mbalimbali kama vile Ajira na Vipato vya wananchi.Hayo yameelezwa Leo mjini Arusha na
Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Dkt Ramadhani Dau wakati akiongea na wadau wa mfuko katika mkutano wa tatu unaoendea mjini hapa.
Dkt Ramadhani alisema kuwa Mfuko huo mpaka sasa umeshaweka Misingi mbalimbali ya kuimarisha zaidi mpango huo wa maendeleo ambapo utaweeza kuraisisha shuguli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kupambana na Umaskini mkubwa sana
Alisema kuwa Mpango huo ambao utaanza hivi karibuni pia utaweza kugusa njaja mbalimbali kwenye jamii hasa nyanja ya uwekezaji wa huduma za msingi kwa Mtanzania kwani utafiti uliofanywa na Mfuko huo umebaini kuwa uwekezaji nao unachangia sana kuimarisha hata uchumi wa Nchi
Mbali na hayo alisema kuwa hata Mapato ya mfuko huo nayo yameongezeka sana tofauti na kipindi cha mwaka 2001 ambapo Mapato yake yalikuwa ni bilioni 39 lakini kwa sasa wamefanikiwa kuvuka katika kiwango cha juu sana hadi kufikia kiwango cha Bilioni 500 kwa mwaka hali ambayo inahitajika kuendeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kupambana na Umaskini.
Awali Waziri wa kazi na Ajira hapa Nchini Gaudencia Kabaka alisema kuwa mfuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini ina nafasi kubwa sana ya kubadilisha maisha ya watanzania hasa kama waaajiri na waajiriwa watakuwa na tabia ya kuchangia mifuko hiyo ya jamii
Kabaka alisema kuwa Mifuko hiyo ya Jamii mbali na kubuni aina mbalimbali za ajira kwa Taifa lakini bado wapo baadhi ya waajiri na waajiriwa ambao hawatii sheria za mifuko hiyo hali ambayo kwa wakati mwingine inasababisha uhaba wa ajira hasa wafanyakazi wanapostaaafu au wanapokabiliwa na matatizo mbalimbali
Tags:
Social
