MAONYESHO YA SHANGAA-ART OF TANZANIA NEW YORK


apo1 ff599
 Sanaa zilizopamba maonesho ya SHANGAA-  Art of Tanzania  ya kwanza na ya aina yake kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani yameandaliwa  na Queens Community Collage moja ya  Vyuo vya Mtandano wa Vyuo Vikuu vya Jiji la New York.(CUNY) kwa kushirikiana na    Dr. Gary Van Wyk,mtaalam wa Historia ya Afrika  amefanya tafiti zake nchini Tanzania na kutokana  mapenzi yake makubwa kwa  Tanzania amempatia mtoto wake jina la Mayala, mwingine aliyeshirikia maandalizi hayo ni    Mkurugenzi wa Art Gallery Bw. Faustino Quintanilla. Maonesho hayo  yaliyokusanya zaidi ya    sanaa 121 kutoka  kwa wadau mbalimbali yalipambwa na  Mhe. Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na aliwashukuru waandaaji wa maonesho hayo kwa uamuzi wao wa kutangaza  mila, tamaduni na  historia nzuri ya Tanzania. Naye Dr. Van Wyk licha ya kuelezea historia nzuri ya Tanzania na watu wake, amewataka washiriki wa maonesho hayo kuitembelea Tanzania  kwa kuwa ni nchi yenye amani, utulivu na watu wenye upendo licha ya tofauti zao za kikabila, dini na rangi

apo2 77316
apo 31dfa

Queense Community Collage ambacho ni sehemu ya mtandao wa Vyuo vikuu vya Jiji la New
York ( City University of New York ) mwishoni wa wiki kiliandaa maonesho sanaa za
kitanzania.
Maonesho hayo yaliyofanyika katika Chuo hicho yanaelezwa na waandaji ni ya kwanza
kufanyika nje ya Tanzania na Ujerumani, yalipewa jina la SHANGAA-Art of Tanzania
likihusisha mkusanyiko sanaa zaidi ya 112 lakini kila moja ikibeba maudhui yake. Kwa kweli
kama lilivyo jina la maonesho hayo, ziliwashagaza wageni mbalimbali waliohudhuria maonesho
hayo.
Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ndiye aliyepamba maonesho
hayo kama mgeni wa heshima, akiambatana na Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania
Nchi Marekani, Bi. Lily Munanka.
Sanaa zilizopamba maonyesho hayo zilikuwa ni za kuchonga nyingi kati yake zikitoka katika
Mikoa ya Usukumani na Umakondeni. Laini pia kulikuwa na video zilizokuwa zikionyesha aina
mbalimbali za ngoma zikionyesha mila na utamaduni wa mtanzania katika uhalisia wake.
Jumla ya sanaa 121 zilikusanywa kutoka wa wadau mbalimbali lakini ni 112 tu zilizoweza
kuoneshwa kutokana na uhaba wa nafasi.
Kwa kutambua umuhimu wa maonyesho hayo Halmashauri ya Jiji la New York ilitoa Hati kwa
waandaaji wa maonesho hayo.
Previous Post Next Post