HALIMA MDEE AONGELEA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE



 Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia”  inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo”
.
Fina Mango akimuuliza Halima Mdee swali wakati wa mahojiano ya moja kwa moja katika kipindi cha Makutano
Mtangazaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango na Mbunge wa Kawe Halima Mdee baada ya kipindi
----
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia”  inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo” . 
  Mdee aliongezea kusema hii yote inachangiwa na mipango ya serikali iliyowekwa kwa kiwango kikubwa sana cha fedha kushindwa kutekelezeka au kusimamiwa ipasavyo ili yaweze kutekelezeka na kutolea mfano wa Mpango waMaendeleo yaElimu ya Sekondari. 
(MMES II) ambao serikali ilitenga Shilingi bilioni 200 wakati huo kiwango cha ufaulu daraja la kwanza hadi la tatu ukiwa 37% ikiwa na malengo kiwango kipande hadi 70% lakini ilipofika 2009 kiwango cha ufaulu kikashuka hadi 17%, 2011 kikashuka tena hadi 9% na mwaka jana kikazidi kudidimia mpaka 5%.  Mdee alisisitiza kuwa tatizo kubwa linalozikabili shule za kata ni miundombinu ya shule na maslahi ya walimu kwa kusema “Kinachojitekeza sasa ni mrundikano wa frustration za walimu, wamekata tamaa kabisa kwa sababu vipato vyao ni vidogo sana, lakini pamoja na kuwa vidogo vile wanavyotakiwa kuvipata kutokana na vipato kuwa  vidogo hawavipati , na zaidi wakati walimu wanasema wanadai serikali inasema hawadai”.

Mheshimiwa Halima Mdee alimalizia kwa kusema anadhani ni wakati sasa kama taifa lazima serikali iamue inataka kufikisha wapi elimu kwa kuwepo bajeti inayotosheleza mahitaji na kuzingatia hali halisi ya maisha na soko,  na kusisitiza uwepo wa mitaala inayoeleweka tofauti na hivi sasa ambapo waalimu wanasema wanapokea maelezo tu na kujiandalia wenyewe mitaala. Pia alisisitiza uwepo wa mgawanyo wa walimu bila upendeleo kwa kila shule tofauti na sasa ambako kuna shule hazina walimu wa kutosha na pia uwepo mamlaka ya usimamizi wa elimu yenye nguvu.
Previous Post Next Post

Popular Items

Magazetini Ijumaa ya Tarehe 23/8/2013