KENYA: WAGOMBEA URAISI WAFANYA MDAHALO KWA MARA YA KWANZA.


Kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya, wagombea urais kwenye uchaguzi ujao nchini humo wameshiriki mdahalo wa pamoja uliohusu mipango yao ya utawala pindi watakapochaguliwa kuongoza serikali.
Mdahalo huo ambao umeonyeshwa moja kwa moja kupitia vituo vyote vinane vya televisheni na zaidi ya vituo 30 vya redio nchini Kenya, umewaleta pamoja wagombea wote wanane wa kinyang’anyiro cha urais, ambao ni Raila Odinga, Uhuru Kenyatta, Musalia Mudavadi, Peter Keneth, James Ole Kiyiapi, Martha Karua ambaye ni mgombea pekee wa kike, Paul Muite pamoja na Mohammed Abduba Dida.
Washiriki wote wanaowania nafasi ya urais wameapa kukubali matokeo ya uchaguzi na ikiwa kuna yeyota ambaye hataridhika atatumia sheria kutoa pingamizi lake badala ya machafuko.
 Masuala mengine kuhusu ukabila, uongozi, ufisadi, usalama, afya na elimu nayo yalijadiliwa kwa kina. Mdahalo mwingine kama huo utafanyika tarehe 25 mwezi huu, wiki moja kabla kufanyika kwa uchaguzi mkuu ujao wa tarehe 4 Machi.

Previous Post Next Post