Joh Makini na G-Nako wafanya wimbo na Sauti Sol wa Kenya

Weusi Joh Makini na G-Nako wanatumia vizuri nafasi walioipata kuwa sehemu ya kipindi cha Coke Studio kinachofanyika Nairobi, Kenya na kuwakutanisha wasanii wakubwa duniani kote.



Wakali hao wamefanya collabo na kundi la Sauti Sol la Kenya, kundi ambalo kimuziki limepiga hatua kubwa hata nje ya Afrika Mashariki. Kazi haikuwa ndogo na iliwabidi wakeshe kuhakikisha inakuwa katika kiwango kinachoridhisha.

“Studioni mpaka alfajiri ya leo na @Sautisol @fancy_fingers @savaramudigi @chimano @bienaimealusa @fundifrank #hakunakulala #Mwenyezi Mungu ni mwaminifu #Kituimepikwa.” Ameandika Joh Makini kwenye post ya Instagram akiwa na G Nako na kundi hilo.

Siku chache zilizopita Joh Makini alifanya collabo na mwanamuziki wa kike kutoka Nigeria Chidinma.
Previous Post Next Post