IDDI AMINI DADA ANYIMWA MEDALI ZA HESHIMA KWA MARAISI WALIOWAHI ONGOZA UGANDA


Idd Amin Dada.
Mwenyekiti wa kamati ya Taifa ya Tuzo na Medali nchini Uganda Jenerali Elly Tumwine ameweka wazi kuwa katika tuzo za heshima zilizotolewa kwa marais waliowahi kuingoza nchi hiyo pamoja na watu wengine ambao mchango wao unatambulika, Aliyewahi kuwa rais nchini humo Hayati Field Marshal Idi Amin Dada hakupata heshima kwa sababu aliacha urithi wa mfumo mbaya wakati wa uongozi wake.
Marais wote wametunukiwa Medali za Miaka 50 ya Uhuru wa Uganda wakati wa maadhimisho ya sherehe za chama cha NRM kutimiza miaka 27 yaliyofanyika wilaya Kasese, ambapo rais Yoweri Museveni alipokea medali ya, sambamba na watu wengine 43.
Jumla ya watu 3,500 nchini Uganda atapokea tuzo hiyo ambayo inawatambua mtu mmoja mmoja kwa mchango wake katika kutoa huduma na uzalendo kwa nchi hiyo tangu ilipopata uhuru.
Jenerali Tumwine amesema Amini hakutambuliwa kwa sababu ya mfumo mbaya aoutumia wakati wa uomgozi wake.
Amini alikuwa rais wa Uganda kutoka mwaka 1971 hadi 1979 ambapo aliingia madarakani kwa kupindua serikali ya Milton Obote Januari 1971.
Marais wengine wote waliopita wakiwemo Sir Edward Mutesa, Obote, Yusuf Lule, Godfrey Lukongwa Binaisa na Gen. Tito Okello, wametunukiwa medali hizo za heshima.
Previous Post Next Post