ECOBANK KUPUNGUZA GHARAMA KATI YA TANZANIA NA CHINA


ECOBANK 4 bbc3f

Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inazidi kukuza uwezo wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki biashara kati ya Tanzania na China kwa kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi. Wakishiriki katika
sherehe ya mwaka mpya ya China Jumapili hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Ecobank ilionyesha nia yake ya kusaidia jamii ya waendesha biashara kati ya Tanzania na China zikiwepo huduma zinazorahisisha wafanyabiashara wa Tanzania na wawekezaji wa Kichina kushiriki katika uagizaji na mauzo ya nje kati ya nchi hizi. "Sisi tunayo nia ya kutoa huduma za garama nafuu na kurahisisha upatikanaji wa bidhaa hizi kuwezesha sekta hii inayokua kwa kasi sana. katika mwongo uliopita kumekuwa na uwekezaji wa $ 868 bilioni wa china ndani ya Tanzania, huduma zetu zinajaza pengo la kurahisisha biashara hii "anasema Bw Enoch Osei-Safo, Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Tanzania.
Ecobank inazindua huduma ya kubadilisha hela ya Tanzania kupata sarafu za kichina (RMB) moja kwa moja, ambapo hapo awali hapa Tanzania, wanabiashara walilazimika kubadili TZS kwa Dola za kimarekani ili kununua RMB. Katika mfumo huo wa awali, wanabiashara walipoteza kiasi kikubwa cha mtaji lakini sasa, Ecobank itatwawezesha wanabiashara kupunguza garama hizi kwa kueneza huduma hii hapa Tanzania.

" Sisi hatuwezi kupuuza matokeo ya biashara ya China juu ya Afrika, ambayo inafikia zaidi ya dola bilioni 200 katika mwaka 2012 kwa uagizaji na 5% ya mauzo yote ya Afrika kwenda nchini China, ushirikishwaji wa kifedha kukuza sekta hii ni muhimu, na ndiyo maana Ecobank Group imeonyesha nia ya kurahisisha uendeshaji wa biashara hii na kuwezesha Afrika kuwa na ushindani na nchi zingine duniani.” Enoch aliongeza.
Ecobank Tanzania katika miezi michache ijayo itakua kituo cha kutoa huduma za uendeshaji biashara kati ya Tanzania na China kwa kutoa huduma ya ubadilishaji wa sarafu ya kichina na pia kulipia kodi ya forodhani kwa TRA papo kwa papo kupitia huduma ya Asybank katika matawi yote ya Ecobank.
Kwa maelezo zaidi, tembelea: www.ecobank.com
Previous Post Next Post