
Afisa habari ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi.Usia Ledama akieleza nia ya Umoja wa Mataifa Tanzania kuendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar juu ya Haki za binadamu na jinsi Mpango wa msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDAP) unavyoshirikiana na Serikali ya Zanzibar katika maeneo matatu muhimu ambayo ni Uchumi, Kupunguza umaskini na Utawala na uwajibikaji. Semina hiyo imefanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View visiwani Zanzibar.

Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan akitoa hotuba ya makaribisho katika mkutano na waandishi wa habari wa Visiwani Zanzibar ambapo amesema wanatarajia kupata mawazo mengi zaidi ya kujenga kutoka kwa waandishi ambapo yatasaidia Umoja wa Mataifa pamoja na Serikali kuihudumia nchi kwa upeo wa juu zaidi.


Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo ambapo ameelezea Mpango Mkakati wa UNDAP visiwani Zanzibar ikiwemo kutoka ufafanuzi wa mafanikio pamoja na changamoto zinazoukabili mpango huo.
Amesema mpango huu ni wa pamoja kwa ajili ya Tanzania unaendena na mafanikio ya malengo ya maendeleo ya kimataifa ambapo unachukua nafasi ya program za pamoja na miradi mingi inayodhaminiwa na UN chini ya Model ya misaada ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa kwa mpango wa kazi moja ulioshikamana kwa ajili ya mifuko ya fedha, program na wakala zote za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.


Katibu wa Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Hamisa Mmanga Makame akitoa somo katika mafunzo hayo ambapo amezungumzia masuala ya Haki za Binadamu, umuhimu wa kuzingatia jinsia na wajibu wa vyombo vya habari katika kuleta usawa.





Pichani Juu na chini ni baadhi ya waandishi ws habari wa visiwani Zanzibar wakichangia mawazo yao wakati wa mafunzo hayo.



Afisa mipango wa Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya siku yaliyoendeshwa na Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar.




Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akijadili jambo na wafanyakazi wenzake wakati wa mafunzo hayo.