MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolper ameandaa filamu mpya atakayoshirikiana na msanii maarufu Elizabeth Michael 'Lulu' itakayokamilika hivi karibuni baada ya msanii huyo kutoka gerezani kwa dhamana
Akizungumza na Maisha Wolpa alisema amepata faraja baada ya taaratibu na sheria kufuatwa na hatimaye Lulu kuweza kupata dhamana hivyo anatarajia kufanya naye kazi ya filamu mpya itakayoanza kurekodiwa baada ya msanii huyo kufika uraiani
Alisema kuwa anatarajia atafanya vizuri katika filamu hiyo kwani tangu awali alikuwa akifanya vizuri katika tasnia hiyo ya uwigizaji kabla ya kupatwa na matatizo
"Nimeshampokea Lulu tangu moyoni mwangu kwani kule alikokuwepo si sehemu nzuri jamani ukiangalia bado ni mtoto mdogo hivyo inaumiza sana" alisema Wolper
Filamu hiyo ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuchezwa na Lulu baada ya kufika Uraiani
Wakati huo huo Rose Ndauka alisema ni wakati wa wasanii kumpokea mwenzao kwani wote ni familia moja na wanahitaji kushirikiana katika kila hali
Alisema kuwa ukiangalia umri wa msanii huyo ni mdogo hivyo ananafasi kubwa bado ya kutengeneza maisha yake na kuangalia wapi amekosea na wapi anapaswa kurekebisha
Naye msanii Single Mtambalike 'Richie Richie' alisema anashukuru kuona sheria imechukua mkondo wake na hatimaye sasa ameweza kuachiwa kwa dhamana hivyo kwa upande wao ni faraja kubwa kwani wote ni familia moja
Alisema anaamini sasa ataweza kujipanga na kufanya kazi vizuri kwani anakipaji na bado wanamuhitaji watanzania kulingana na uwezo mkubwa alionao kwenye tasnia hiyo