KINONDONI WAPATIWA VIFAA VYA KUTUNZIA TAKA



002
Meneja Mikopo wa BankABC, Eugenia Shayo akikabidhi sehemu ya vifaa 100 vya kubebea taka kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda vyenye thamani ya sh milioni 3.5.
003
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.

Manispaa ya Kinondoni imekabidhiwa vifaa 100 vya kutunzia taka na benki ya BankABC vyenye thamani ya shilingi milioni 3.5 leo Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Meya wa Manispaa hiyo, Yusuph Mwenda amesema Manispaa yake itahakikisha usafi unazingatiwa na mkazi atakayebainika kutupa taka ovyo atachukuliwa hatua kali ikiwemo kumtoza faini ya kuanzia shilingi 50,000 mpaka 10,000 “Hii ni kampeni maalumu
tuliyoizindua ya kuweka safi Mazingira ya Manispaa yetu. Sasa natoa wito kwa wakazi wa Manispaa kuvitunza vifaa hivi sambamba na kuyatunza mazingira vinginevyo haitasita kuwatoza faini. Na faini yetu itaanzia shilingi 50,000 hadi shilingi 10,000.” Alisema.
 Naye Ofisa Masoko wa benki hiyo, Evelyn Auguste amesema wameamua kushirikiana na Meya huyo baada ya kuvutiwa na kampeni hiyo ya utunzaji wa Mazingira.
Previous Post Next Post