KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO IKIWEMO SOKO LA KIMATAIFA LA PAMOJA MKOANI KIGOMA





Jengo la Soko la Pamoja lililokaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo jioni,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bw. Juma Magango akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokwenda kukagua Soko la Pamoja  leo jioni.  
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma  Magango (shoto) na baadhi ya Wanachi wakielekea kukagua  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.

Wakielekea kukagua ujenzi wa mradi wa darja la pamoja.
Pichani ni  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.

Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika februari 20,2013 utagharimu kiasi cha shilingi 260,000,000/=,aidha imeelezwa kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu nne,awamu ya kwanza imeshaanza ambayo unahusisha ujenzi wa daraja,barabara KM1 inayotoka kwenye soko hadi darajani na hifadhi ya Mazingira,utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia 70% mpaka sasa.

Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai alipokwenda kukagua mradi  wa ujenzi wa  daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai akitoa ufafanuzi mbele ya Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana kuhusiana na ujenzi wa Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye shule ya sekondari ya Nyamtukuza iliopo kwenye Wilaya ya Kibondo,mkoani Kigoma,pichani shoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango wakikagua ujenzi wa shule hiyo ya  Nyamtukuza 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kushoto akishiriki kwenye ujenzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana,kulia kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza mapema jioni ya leo,Kinana aliuahidi uongozi wa shule hiyo kuwapa umeme (Solar Pannel )mbili kwa ajili ya kuzalisha umeme shuleni hapo,Kampyuta moja pamoja na Televishen
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipokelewa na wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutanno wa hadhara mapema leo jioni na Wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Sehemu ya shamba la Mahindi safi kabisa,ambalo pia Ndugu Kinana aliwahimiza wanakijiji cha Rumashi,kutumia Pembejeo za mbolea kuhakikisha wanapata mazao bora. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko mapema jana jioni.

Previous Post Next Post