Viongozi wa ngazi ya juu wa Jeshi la Magereza, ugeni kutoka nchini Vietnam pamoja na wageni mbalimbali walioalikwa katika sherehe hiyo wakigongesha vinywaji vyao ikiwa ni ishara ya kufurahi kuwepo pamoja katika eneo hilo.
Rais wa Kiwanda cha Kutengeneza Kofia ngumu za kisasa (Helmet) kilichopo nchini Vietnam, Greig Craft (kulia) akimpa zawadi Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (wa pili kutoka kulia) akitoa shukrani kwa ugeni kutoka nchini Vietnam kwa kuitikia mwaliko wa kupata chakula cha jioni. Kulia ni Hoang Thi Na Huong, Naibu Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu (Helmet) kilichopo nchini Vietnam. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna Edita Mallya. Anayefuata ni Rais wa Kiwanda cha Kutengeneza kofia ngumu za kisasa nchini Vietnam, Greig Craft, na wa katikati ni Gaston Sanga, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza.
Wageni waalikwa wakishiriki chakula cha jioni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali John Minja.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (katikati) akimtambulisha Gaston Sanga, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza kwa ugeni kutoka nchini Vietnam. Wa pili kutoka kushoto ni Deonice Chamulesile, Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Magereza. Ugeni huo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza wanatarajia kujenga kiwanda cha kofia ngumu za kisasa (Helmet) nchini hivi karibuni ili kuzuia ajali mbalimbali zinazotokana na pikipiki.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akifurahia jambo na Rais wa Kiwanda cha Kutengeneza kofia ngumu za kisasa nchini Vietnam, Greig Craft.
PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI