Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akiwaonyesha cheti cha Ukaguzi wa Mazingira ambacho hupatiwa Wamiliki wa Mahoteli na viwanda. Waziri Huvisa alikuwa akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini Kwake Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga.
Na Heka Wanna na Shakila Galus,MAELEZO
Serikali  ya Tanzania imesema itaanza mchakato wa kuridhia itifaki mpya ya Kyoto ili nchi na wananchi waweze kuendelea kunufaika na fursa zilizopo chini chini ya mkataba huo.
Kauli hiyo imetolewa  jijini na WAZIRI wa Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Mhe.Dkt.Terezya Huvisa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu walichojadili katika mkutano wa 18 wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi uliofanyika Doha nchini Qatar.            
Alisema kuwa mkutano huo ulilenga kujadiliana  jinsi ya kukubaliana  upunguzaji wa gesi joto kwa nchi zilizoendelea kwa asilimia 25-40 .
Dkt. Huvisa aliongeza kuwa chini ya itifaki hiyo nchini zinazoendelea zitaweza kunufaika na miradi ya kupunguza gesijoto (CDM) na Mfuko wa kuhimili mabadiliko  ya tabianchi inayogharmiwa na Nchi zilizoendelea.
Alisema kuwa chini ya utekelezaji wa itifaki utawezesha nchi husika kupata fedha za kusaidia  uharibifu wa misitu.
Aidha aliongeza kuwa miradi  ya CDM inayotekelezwa katika nchi maskini kama Tanzania itaendelea kusamehewa kuchangia 2% kwenye mfuko wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi ili kuwezesha nchi maskini kuwa na miradi mingi na kupunguza gharama za uwekezaji na utekelezaji wake na kuchangia maendeleo endelevu.
Dkt.Luogya aliendelea kwa kusema  awamu ya kwanza utekelezaji wa mkataba wa kyoto utamalizika tarehe 31 Disemba mwaka huu (2013) na awamu ya pili ya utekelezaji itaanza ifikapo tarehe 1 januari 2013