Mfalme wa Japan Akihito amemwapisha Shinzo Abe (pichani) kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo.Muda mfupi baada ya bunge kumpigia kura ya kuwa waziri mkuu mpya, Abe alitangaza baraza lake jipya la mawaziri.
Waziri mkuu huyo mwenye umri wa miaka 58 ameingia madarakani kwa ahadi ya kupambana na ughali wa maisha na kuufufua uchumi wa Japan unaoyumba.
Abe amerudi tena katika uongozi wa nchi hiyo kwa mara ya pili baada ya kuongoza katika mwaka wa 2006.
Shinzo Abe pia ameahidi kulipa kipau mbele suala la kuiamrisha uhusiano wa Japan na Marekani.
Ametangaza mpango wa kichocheo cha uchumi wa takribani euro bilioni 90 ili kuufufua tena uchumi wa Japan, unaokuwa polepole.

Tags:
Uncategolized