HII NDIYO OFISI YA CCM KISHUMUNDU NI BALAA


Hili si zizi la Mbuzi au banda la kuku bali ni Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyopo  Kijiji cha Kiaseni Kata ya Kishumundu, Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro. Ofisi hii  iliyopo katika jimbo la Mbunge Thirili Chami ni miongoni tu mwa ofisi nyingi za chama hicho katika vijiji vingi nchini ambazo zipo katika hali mbaya  huku baadhi ya Vijiji Kama kile cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali,  Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro vikiwa havina kabisa Majengo ya Ofisi za chama hicho Tawala jambo ambalo linaathiri utendaji wa Viongozi wa Chama ambao ndio wameshikilia mhimili wa kuiongoza dola.

Previous Post Next Post