UNITED NATION TANZANIA YAHAMAMSISHA UPANDAJI MITI.


 Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Bw. Austin Makani akizungumza na wakazi wa kata ya Pugu akizungumzia kwanini Umoja wa Mataifa katika wiki hii ya maadhimisho ya miaka 67 tangu kuanzishwa pamoja na mambo mengine imeamua kutilia mkazo suala la Utunzaji wa Mazingira kwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu unapozungumzia suala zima la  kutoa elimu juu ya mabadiliko ya Tabia nchi
 Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro (wa pili kulia) aliyemwakilisha mgeni rasni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,  Bi. Stella Karegesya UNV Program Officer Tanzania (kulia) Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Fresh Bw. Ally Maguno, Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw. Justin Nyangwe na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kinyamwezi Bw. Mohamedi Abdalah aliyemwakilisha Diwani wa Kata ya Pugu katika meza kuu
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Pugu Bw. Justin Nyangwe akizungumza wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi ambapo ametoa shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuwapa umuhimu wakazi wa Pugu kwa kuchukua hatua ya kushirikiana nao katika suala zima la kuboresha mazingira na wanaahidi kuwa mfano wa kuigwa katika utunzaji wa mazingira
 Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro (wa pili kulia) aliyemwakilisha mgeni rasni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akitoa nasaha zake katika wiki ya maamdhisho ya Umoja wa Mataifa ambapo Umoja huo ulikwenda kufanya kampeni ya kuhimiza wananchi kutunza mazingira katika Kata ya Pugu
Previous Post Next Post