Sasa ni ‘Lady Jaydee and the Band’ na sio Machozi Band tena ...

Mwanadada Lady Jaydee hajabadilisha jina la lounge yake kutoka Nyumbani Lounge hadi MOG peke yake. Machozi Band kwa sasa nayo itakuwa ikijulikana kama ‘Lady Jaydee and the Band!’


“Tumeondoa kulia,” Lady Jaydee amekiambia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio.

Katika hatua nyingine Jaydee amezungumzia wimbo wake mpya ‘Forever’ aliomshirikisha mdogo wake Dabo. Wimbo huo umetayarishwa na Man Walter wa Combination Sound.

“Mwezi wa kumi na moja mwishoni natoa nyimbo mpya pamoja na video. Wimbo unaitwa Forever nimemshirikisha Dabo mdogo wangu, toka mimi kuzaliwa ananifuata yeye. Yeah ni ngoma ya kwanza nilikuwa namuacha apevuke kwanza akue na ajisimamie,” alisema Jaydee.
Previous Post Next Post