Samsung kuja na teknolojia ya WiFi itakayomuwezesha mtumiaji wake kudownload movie ya 1GB kwa sekunde 3!

Kampuni ya Samsung ya Korea Kusini imetengeneza teknolojia ya 60 GHz ya WiFi ambayo itaweza kutuma data mara tano zaidi ya vifaa vingine.



Kifaa hicho kitakuruhusu kutuma data zenye ukubwa wa megabytes (MB) 575 kwa sekunde 1 – ambapo ni sawa na kudownload filamu ya GB 1 kwa sekunde 3 tu.

Hiyo inamaanisha kuwa video zenye ukubwa na za high-definition zinaweza kuangaliwa kutoka kwenye simu kwenda kwenye TV katika muda huo huo real-time.

Teknolojia ya Wi-Fi iliyopo sasa ni ya 2.4 GHz na 5 GHz.

Source:Samsung
Previous Post Next Post