Mama Huyu aamua kukatisha maisha ya mwanae kwa kumpunguzia mateso

Mama ameweka historia kwenye sheria baada ya kushinda kesi Mahakama Kuu ya kukatisha maisha ya binti yake mwenye umri wa miaka 12.

Nancy Fitzmaurice alizaliwa kipofu na akisumbuliwa na haidrofalisi, matatizo ya uti wa mgongo na ubongo, matatizo ya damu, yaliyomfanya ashindwe kuzungumza, kutembea, kula na kunywa.


Nancy Fitzmauric alizaliwa kipofu, hawezi kula, kunywa, kutembea wala kuongea.

Maisha yake yalikuwa duni sana akitegemea msaada wa hospitali wa kulishwa, kunyeshwa maji na kupewa dawa kwa mirija kwenye Hospitali ya Great Ormond iliyopo jijini London.


Nancy alifariki August 21 baada ya madaktari kuondoa chakula na maji.

Ila wakati alipoondolewa utaratibu huo ambao ulimuacha akilia kwa maumivu makali, mama yake Charlotte Fitzmaurice, aliamua kukatisha kumuangalia mwanaye, na hivyo kufanya maamuzi ya kuumiza moyo wake kwa kukatisha maisha ya Nancy.


Hospitali ya Great Ormond ya jijini London ambako Nancy alikuwa akipatiwa matibabu wakati wa uhai wake.

Katika kesi hiyo, Mtaa wa Great Ormond ulipigana kwa niaba ya Charlote, na baba David Wise, kumpa haki ya kukatiza maisha yake.

Inadaiwa kuwa miaka ya nyuma vitendo hivi vilikuwa viifanywa na wakunga, walipoona kuwa mtoto aliyezaliwa ana ulemavu ambao ungemtesa maishani mwake, waliona ni bora auawe na kudai mtoto hakuwa rizki.
Previous Post Next Post