Lundenga ashinda kesi ya kuendelea kuendesha shindano la Miss Tanzania, Oct 11

Mwanzilishi Mwenza wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga ameshinda kesi ya kuendelea kuendesha shindano hilo baada ya kufunguliwa mashtaka na mwenzake Prashant Patel ili kusitisha kufanyika kwa shindano hilo lililopangwa kufanyika October 11 kwenye ukumbi wa Mlimani City.


Akizungumza na waandishi wa habari leo, Lundenga amesema hakimu aliyekuwa akisimamia kesi hiyo ameamua kuifuta.

“Kuanzia juzi magazeti yamekuwa yakiripoti suala lilokuwepo mahakama ya Kisutu, kwamba mashindano ya Redd’s Miss Tanzania 2014 yatapata ‘court injunction’. Yameripoti sana na ukitaka kujua kitu chetu kikubwa media zote zimeripoti,” amesema Lundenga.

“Baada ya kuripoti jana na leo magazeti yameendelea kuripoti vitu ambavyo naweza kusema havikuwa sahihi sana. Kilichotokea jana ni kwamba baada ya sisi au mimi kwamba Patel ana kusudio la kuzuia shindano, mimi na mwanasheria wangu tukatoa objection ya lile kusudio ambayo inaitwa ‘preliminary objection’ sasa kupitia preliminary objection majibu yake yamepatikana saa 2:30 na hakimu alikataa mimi kutokusikilizwa.”

Kwahiyo tukaingia awamu ya jioni kuanzia saa tisa tukaingia tena katika kusikiliza shauri hilo na baada ya kusikiliza shauri hilo hakimu ameamua kutupilia mbali hoja ya Patel ya kutaka kuzuia shindano. KwaHIyo mimi nimeshinda na mpaka sasa mashindano yanaendelea kama kawaida.”

Katika kesi hiyo, pamoja na mengine, Patel alikuwa akitaka pia kulipwa fedha zake shilingi milioni 19 kutoka kwa Lundenga.

Source:MichuziBlog
Previous Post Next Post